Kiongozi Muadhamu akutana na familia za mashahidi wa uovu wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo amekutana na familia za mashahidi wa Jeshi la Ulinzi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran waliouawa shahidi katika uovu wa hivi karibuni wa utawala wa Kizayuni.

Akizungumza na familia za mashahidi hao, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema kuwa, hadhi na daraja ya mashahidi hao ni ya juu.

Kiongozi Muadhamu amesema, mashahidi wote wako katika daraja nzuri kando ya neema za Mwenyezi Mungu, lakini kuuawa shahidi wapendwa wa familia hizi ni kufa shahidi ambako ni adhimu, kuliko na daraja ya juu na muhimu kutokana na kazi yao ya ulinzi wa nchi na taifa katika makabiliano ya moja kwa moja na utawala wa Kizayuni ambao ni adui khabithi na muovu zaidi wa Uislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia ameziombea subira na utulivu wa moyo familia za mashahidi hao na kuongeza kuwa: Malipo ya familia za mashahidi si kidogo kuliko mashahidi.

Askari wanne wa kikosi cha anga cha Iran waliuawa shahidi katika shambulio la Israel la Oktoba 26 dhidi ya Iran.