Kinshasa yashtumu UNSC kwa kutochukuwa hatua baada ya kutekwa kwa Bukavu

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) siku ya Jumatatu imeshutumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusindwa kuchukuwa hatua sikumoja baada ya kundi la waasi la M23 wanaoshirikiana na jeshi la Rwanda kuteka mji wa Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, kulingana na barua ambayo AFP imepata kopi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Serikali yangu imekasirishwa kuona kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lililodhoofika na ugonjwa usiojulikana, halikuweza kuchukua uamuzi, licha ya uzito wa hali,” ameandika balozi wa Kongo katika Umoja wa Mataifa Zénon Mukongo Ngay katika barua hii iliyotumwa kwa Baraza hilo.

“Kupooza” huko kumetoa “utawala huru wa kuendelea kukalia kwa mabavu maeneo ya Kongo na Wanajeshi wa Ulinzi wa Rwanda na wasaidizi wao kutoka kwa kundi la kigaidi la M23,” ameongeza.

“Haishangazi, tabia ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kushindwa kuchukuwa hatua, tabia hiyo imesaidia tu kuendeleza hali mbaya zaidi, na kusababisha kutekwa” kwa Bukavu, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, ameshutumu, pia akiishutumu Rwanda kuwa “maabara ya ukosefu wa utulivu katika eneo la Maziwa Makuu”.

Baada ya kuiteka Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, katika mashambulizi makali mwishoni mwa mwezi wa Januari, M23 na wanajeshi wa Rwanda waliendelea kusonga mbele katika mkoa jirani wa Kivu Kusini na mji wa Bukavu, ulioanguka mikonini mwao siku ya Jumapili.

Katika muktadha huu, balozi wa Kongo anaomba katika barua yake mkutano mpya wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC), ambao anautaka kuchukua hatua yenye “maamuzi na ya haraka”.

Kama ilivyofanya mwezi mmoja uliopita, Kinshasa inatoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kudai kuondolewa kwa wanajeshi wa Rwanda katika ardhi ya Kongo. DRC pia inasisitiza madai yake ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Kigali, hasa vikwazo vya kibinafsi dhidi ya maafisa wa kisiasa na kijeshi wa Rwanda, na kuzuiwa kwa mauzo ya maliasili kutoka Rwanda.