#KIMATAIFA: Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina, amejiuzulu wadhifa wake kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo

#KIMATAIFA: Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina, amejiuzulu wadhifa wake kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo.

Waziri Mkuu Sheikh Hasina, amejiuzulu na kuondoka katika Mji Mkuu (Dhaka) wakati kukiwa na maandamano makali ya kumtaka ajiuzulu, ambapo wasiopungua 90 wameuawa nchini humo, huku kukiwa na mapigano makali kati ya polisi na waandamanaji wanaoipinga serikali.

Uamuzi huo umekuja ikiwa ni muda mfupi tangu Umoja wa Mataifa uitake Serikali kusitisha mara moja machafuko yanayoendelea Nchini humo ambayo yamesababisha vifo wakiwemo Maafisa wa Polisi.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania.

#Follow @radioonetanzania