
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameishutumu Marekani kwa kuongeza mivutano na uchokozi na kueleza kwamba, amesema rasi ya Korea haijawahi kukabiliwa na hatari ya vita vya nyuklia kama sasa.
Katika hotuba yake kwenye maonyesho ya kijeshi mjini Pyongyang, Kim alisema uzoefu wake wa awali wa mashauriano na Washington ni kuangazia sera yake ya “uchokozi na uadui” dhidi ya Pyongyang.
Wakati wa utawala wa Rais-mteule Donald Trump, Trump na Kim walifanya mikutano mitatu isiyo ya kawaida huko Singapore, Hanoi,na mpakani mwa Korea mwaka 2018 na 2019, imeshindwa kufanikisha matokeo yoyote maana.
Kim katika hotuba yake ametaka kuendeleza na kuboresha silaha kuwa za “kisasa zaidi” na kuapa kuendelea kuboresha uwezo wa ulinzi na kuimarisha nafasi ya kimkakati ya nchi hiyo.
Hotuba ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini imekuja kufuatia ukosoaji wa kimataifa kuhusu ongezeko la ushirikiano wa kijeshi kati ya Pyongyang na Moscow, wakati Korea Kaskazini ikiwa imetuma zaidi ya wanajeshi 10,000 kwenda Russia kuisaidia katika vita vyake dhidi ya Ukraine.