Kikao cha tano cha Kamisheni ya Pamoja ya Iran na Tanzania kimeshirikisha wanawake wengi

Makamu wa Rais wa Iran anayehusika na Masuala ya Wanawake na Familia ametangaza kuwa kikao cha tano cha Kamisheni ya pamoja ya Iran na Tanzania kimefanyika kwa kushirikisha wanawake wengi na kwa lengo la kupanua uhusiano wa kiuchumi, kibiashara, kijamii na kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa mtandao wa Sahab ukinukuu shirika la habari la IRNA, katika kikao hicho kilichofanyika kuanzia tarehe 16 hadi 19 Oktoba 2024 jijini Dar es Salaam, hati kadhaa za makubaliano na ushirikiano zilitiwa saini kwa lengo la kuimarisha na kupanua uhusiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Moja ya sifa maalumu iliyokuwa nayo kamisheni ya pamoja ya  Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Tanzania ni uwepo wa wanawake kutoka nchi zote mbili katika nyadhifa za uongozaji wa kamisheni, ambapo Bi Maryam Jalili Moghadam, Naibu waziri na mkuu wa Shirika la Utunzaji Mimea la Iran, aliongoza ujumbe wa Iran kama mkuu wa utendaji wa ujumbe huo, na katika vikao vya mwisho vya maandalizi ya hati za makubaliano.

Kadhalika, katika uundaji wa kamati tatu za uandaaji wa hati za makubaliano, Elham Savalanpour, Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Utamaduni na Kijamii katika ofisi ya Makamu wa rais wa Masuala ya Wanawake na Familia wa Iran, ameongoza kamati ya utamaduni na kijamii, na ndiye aliyekuwa na jukumu la kuandaa waraka huo.

Katika fremu ya kuwa na maelewano chanya na nchi mbalimbali duniani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijifungi na kufuata mwelekeo wa upande mmoja tu wa kujenga mashirikiano na nchi za Ulaya pekee, bali inatilia mkazo pia kuwa na uhusiano wa karibu na nchi za mabara ya Afrika na Asia…/