Kikao cha mawaziri wa AU chamalizika kwa mwito wa maendeleo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika wamemaliza Kikao chao cha 46 cha Kawaida cha Baraza la Utendaji la Umoja wa Afrika (AU) kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Ethiopia na kutoa mwito wa kuendelea kupigania maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii barani humo.