
CHAMA cha Kikapu Mkoa wa Kigoma kimetamba kuwa na viwanja wanaochipukia katika mchezo huo ambao ni toleo jipya linalotarajiwa kuwa kutisha siku za usoni.
Katibu wa chama hicho, AQ Anasi ameliambia Mwanaspoti kuwa mwamko umekuwa mkubwa kwa vijana wanaojifunza kucheza kikapu.
Anasi ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya vijana umri wa miaka 16, alisema mwamko unatokana na ushirikiano kati chama hicho na shule mbalimbali ambako vipaji vipaji vimeibuka. “Licha ya viwanja kuwa vichache vijana wamekuwa wakijitokeza wengi na wanaojitokeza wanapewa mafunzo,” alisema.
Alisema wataendelea kutembelea shule ili kuwahamasisha vijana wajifunze mchezo huo kwa sababu ni ajira. Wakati huohuo, alisema uongozi wa chama utakapokutana wakati wowote kuanzia sasa watajadili kuhusiana na ligi inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.
“Tumejipanga katika ligi hii tuwe na wadhamini watakaotusapoti… mwaka huu tumejipanga kufanya hivyo,” alisema Anasi na kuongeza tayari wameshaanza kuzungumza na wadhamini ambao wameonyesha nia ya kudhamini ligi hiyo.