Khatibu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Trump hatafikia malengo yake kuhusiana na Iran

Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, Rais Donald Trump wa Marekani anatoa vitisho na kuainisha kikomo cha uwezo wa nyuklia wa Iran na ushawishi wake katika eneo lakini anakosea na hatofikia malengo yake.