Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran alisifu Bunge lilivyoamiliana vizuri na Serikali mpya

Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amesema, kupigiwa kura ya imani mawaziri wote na Bunge la 12, ambayo ni hatua nadra kuwahi kushuhudiwa kunaonyesha jinsi Bunge hilo lilivyoamiliana kwa busara na kitaalamu na Serikali mpya ya 14.