Kevin Farrell, rafiki wa karibu wa Papa Francis, kukaimu nafasi ya papa

Tangu kifo cha Francis, amekuwa mtu mashuhuri. Kadinali Mmarekani mwenye asili ya Ireland Kevin Farrell, kama Camerlengo, anawajibika kusimamia masuala ya kila siku ya Vatican, akisubiri kuchaguliwa kwa papa mpya. Camerlengo ni msimamizi wa mali na mapato ya Vatican. Ni kazi yake kutekeleza itifaki na kuandaa mazishi.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Wakati Papa Francis alimpa nafasi ya camerlengo mnamo mwaka 2019, ambayo ni kusema, kama camerlengo ya muda baada ya kifo chake, Kevin Farrell, akiwa na shauku ya kumuona Papa akiwa hai kuliko yeye, alijibu kwa mzaha: “Ndiyo, kwa sharti moja kwamba usimamiye mazishi yangu mwenyewe!” “Sentensi inayosema mengi kuhusu ushirikiano kati ya watu hao wawili.

Kevin Farrell, 77, mzaliwa wa Dublin, Ireland, alisoma Hispania na kisha Italia, ambako alipata shahada ya falsafa na teolojia kabla ya kutawazwa kuwa kasisi mwaka 1978. Kisha akavuka Atlantiki, akihudumu Mexico kama kasisi katika Chuo Kikuu cha Monterrey na kisha Marekani, ambako alitumia miaka 30 ya maisha yake. Alipanda ngazi, akawa Askofu Msaidizi wa Washington, kisha Askofu wa Dallas.

Mnamo mwaka wa 2016, Papa Francis alimleta Roma kuongoza dicastery mpya, sawa na huduma, kwa Walei, Familia na Maisha. Kevin Farrell anajulikana kwa msimamo wake. Katika mahojiano ya 2022 na jarida la Jesuit la America, alisema anapenda “kuwaweka watu wanaofaa mahali pazuri.” Walei badala ya mapadre katika usimamizi wa dayosisi. Na kuhusu matayarisho ya ndoa, yeye anasema, “tunapaswa kutegemea zaidi wenzi wa ndoa ambao wamejitolea, badala ya kuwategemea tu makasisi ambao wana maono ya kweli na wasio na uzoefu.”

Muda mfupi baada ya kushika wadhifa huo mjini Roma, Papa Francis alimteua kuwa kadinali na kumkabidhi majukumu mengine, kama vile uenyekiti wa Tume ya Masuala ya Siri mwaka 2020 na kusiamia Mahakama Kuu ya Vatican mwaka 2023. Lakini bila shaka ni kwa kumkabidhi wadhifa wa camerlengo ambapo Papa Francis alionyesha imani yake kubwa kwake.

Ubaya pekee ni kwamba Kevin Farrell alihudumu kwa miaka kadhaa chini ya Askofu Mkuu wa Washington Theodore McCarrick, ambaye alishutumiwa kwa kuwanyanyasa watoto kingono katika miaka ya 1970. Kisa hicho kilidhihirika mwaka wa 2018. McCarrick alifukuzwa kazi mwaka wa 2019 na alifariki hivi majuzi. Kevin Farrell anadai kuwa hajawahi kujua chochote kuhusu dhuluma hizi. Katika mahojiano na National Catholic Reporter, Julai 24, 2018, alisema: “Nilishtuka, nilizidiwa, sikuwahi kusikia kitu kama hiki katika miaka sita niliyokaa naye.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *