Kesi ya wahudumu wa afya ya Diego Maradona haiwezi kuendelea nchini Argentina baada ya kubainika kuwa jaji aliyehusika katika kesi hiyo alishiriki katika makala kuihusu.
Hakimu anayesimamia kesi hiyo iliyoanza Machi 11 na ilitarajiwa kuendelea hadi Julai, alisema italazimika kuanza tena.
Wanachama saba wa timu ya matibabu ya Maradona walishtakiwa kwa mauaji ya kizembe yanayohusiana na kifo cha mwanasoka huyo wa zamani mnamo mwaka 2020.
Hata hivyo, wamekanusha madai hayo.
Mmoja wa majaji watatu wasimamizi, Julieta Makintach, alijiuzulu wiki hii.
Maradona, kiungo wa zamani wa Napoli na Argentina, alikuwa akipata nafuu nyumbani kwake Buenos Aires kutokana na upasuaji wa ubongo wa kuganda kwa damu mnamo mwezi Novemba 2020 alipofariki kutokana na mshtuko wa moyo, akiwa na umri wa miaka 60.
Miongoni mwa timu ya matibabu ni mtaalamu wa mfumo wa neva, daktari na muuguzi wa usiku.
Wanadai mwanasoka huyo aliyestaafu alikataa matibabu zaidi na alipaswa kukaa nyumbani kwa muda mrefu baada ya upasuaji wake.
Iwapo watapatikana na hatia, wanakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka minane hadi 25 jela.
#StarTvUpdate