KESI YA LISSU UPDATES: Polisi ilivyodhibiti mikusanyiko Kisutu, usalama waimarishwa

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limedhibiti eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ambako umati wa wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), umefika kufuatilia kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wao, Tundu Lissu.

Katika maeneo yote ya mahakama hiyo, polisi wenye silaha, mbwa na farasi wameonekana wakiimarisha ulinzi tangu alfajiri hadi saa tatu wakati kesi hiyo inayosikilizwa kwa njia ya mtandao ilipoanza.

Polisi wakiimalisha ulinzi nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Picha na Michael Matemanga

Hadi kufikia saa 3 asubuhi, hakuna kikundi cha watu kilichokuwa kwenye eneo hilo la mahakama na jirani zaidi ya waandishi wa habari ambao wameruhusiwa kusimama umbali wa kama mita 100 kutoka lilipo geti la mahakama.

Polisi wakiimalisha ulinzi nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. Picha na Michael Matemanga

Polisi hao wametoa amri na kutaka kila mtu aendelee na shughuli zake.

Hata hivyo, waliokwenda kinyume na maagizo hayo wametiwa mbaroni na wengine wakipewa onyo.

Lissu anakabiliwa na kesi mbili, moja ya uhaini na nyingine ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni. 

Kwa mara ya kwanza Lissu alipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo, Aprili 10, 2025. 

KESI YA LISSU UPDATES: Mtandao changamoto,hakimu aahirisha kwa muda 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kwa muda kesi ya kusambaza taarifa za uongo katika mtandao wa Youtube inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu.

Uamuzi huo umetolewa leo, April 24, 2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geoffrey Mhini wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa njia ya video, ili mshtakiwa asomewa hoja za awali.

Hakimu Mhini amesema kutokana na mtandao kusumbua, anaahirisha kwa muda na kama utakuwa bado kuna changamoto atatoa uamuzi.

Hata hivyo, ukumbi huo wa video conference uliopo katika Mahakama hiyo, umejaa hali iliyosababisha baadhi ya watu kuzuiwa kuingia.

Endelea kutembelea mitandao ya kijamii ya Mwananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *