Kesi ya ICC juu ya Duterte ina nguvu za kutosha kwa kuhukumiwa, anasema wakili William Bourdon

Mawakili wa Rodrigo Duterte, ambao wako njiani kuelekea Hague kukabiliana na mashtaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), wamewasilisha ombi la kutaka arejeshwe Manila. Rais huyo wa zamani wa Ufilipino alihamishiwa Uholanzi na kukabidhiwa kwa ICC siku ya Jumatano, Machi 12, taasisi hiyo metangaza, ikiongeza kuwa kikao cha kwanza cha kusikilizwa kitaratibiwa kwa wakati ufaao. Anaweza kuwa mkuu wa kwanza wa zamani wa nchi ya Asia kuhukumiwa na ICC.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Kwa familia za waathiriwa wa umwagaji damu wa Rodrigo Duterte alipokuwa mamlakani, kukamatwa huku kunafufua matumaini ya haki. Makumi ya maelfu ya watu waliuawa katika operesheni za kupambana na dawa za kulevya zilizoanza mwaka wa 2016, idadi ambayo inaweza, kwa kweli, kuwa kubwa zaidi.

Kulingana na wakili wa uhalifu William Bourdon, kesi hiyo ina nguvu za kutosha kwa rais huyo wa zamani wa Ufilipino kuhukumiwa. “Mwendesha mashitaka ni mtu aliyejitolea sana. Kuna ushuhuda mwingi ambao umekusanywa: mashirika mengi yasiyo ya kiserikali nchini Ufilipino yamekuwa yakitumia mbinu za kukusanya, kupanga, na kutafsiri shuhuda kwa miaka mingi, anaelezea wakili aliyewasiliana na Anne Verdaguer wa kitengo cha kimataifa cha RFI. Nadhani tunaweza kuwa na uhakika kwamba kiongozi huyu wa zamani wa Ufilipino atatiwa hatiani kwa uhalifu ambao alifanya, kupanga, kudaiwa, na kubuni dhana alipokuwa ikulu ya rais huko Manila. “

Duterte achukua jukumu la kupambana na dawa za kulevya

Mwendesha mashtaka Karim Khan alisema kutekelezwa kwa hati ya kukamatwa kwa Rodrigo Duterte ni muhimu kwa waathiriwa. Sheria za kimataifa sio dhaifu kama wengine wanavyofikiria, aliongeza, muda mfupi baada ya Rodrigo Duterte kuhamishiwa Hague. Katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, rais huyo wa zamani wa Ufilipino alisema alichukua jukumu kamili la vita dhidi ya dawa za kulevya, akieleza kuwa, “kuwalinda” raia wake, ndiye “aliyeongoza vikosi vya usalama na jeshi.” “Niliwaambia polisi, jeshi, kwamba ilikuwa kazi yangu na kwamba ninahusika nayo,” aliongeza.

Utekelezaji wa hati ya kukamatwa kwa ICC “ni muhimu kwa waathiriwa. “Nadhani ina maana kubwa kwao,” Karim Khan alisema katika taarifa baada ya Rodrigo Duterte kukabidhiwa kwa mahakama. “Watu wengi wanasema kuwa sheria ya kimataifa haina nguvu kama tunavyotaka, na ninakubali. Lakini kama ninavyosisitiza mara kwa mara, sheria ya kimataifa si dhaifu kama watu wengine wanavyofikiri, mwendesha mashtaka aliongeza. Tunapoungana (…) utawala wa sheria unaweza kutawala. “

Rodrigo Duterte alikabidhiwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu siku ya Jumatano, Machi 12, alipowasili Uholanzi, mahakama hiyo ilitangaza siku ya Jumatano, baada ya kutoa hati ya kukamatwa kwa rais huyo wa zamani wa Ufilipino kwa madai ya uhalifu wakati wa vita vyake dhidi ya dawa za kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *