
Kesi iliyowasilishwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dhidi ya Rwanda mbele ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR), huko Arusha, nchini Tanzania, imeanza kusikilizwa. Mjadala katika hatua hii unajikita tu kwa maswali ya muundo. DRC inashutumu jirani yake kwa ukiukaji wa haki za binadamu, ukiukaji wa mipaka na mauaji katika mkoa wa Kivu Kaskazini tangu mwaka 2022.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
DRC ilitangaza Jumatatu, Desemba 2, 2024 kwamba itaifungulia mashitka nchi jirani ya Rwanda katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Kibinadamu na Watu, ambayo ni mamlaka iliyo chini ya Umoja wa Afrika yenye makao yake makuu mjini Arusha, nchini Tanzania.
Mkakati wa mawakili wa upande wa Rwanda unalenga kwanza kuonyesha kwamba mahakama ya Afrika haina uwezo wa kushughulikia kesi hii, anaripoti mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa. Wanataka mahakama hiyo ijitangaze kuwa haina uwezo wa kusuluhisha mzozo huu au kutangaza hatua ya Kongo kuwa hakikubaliki. Mawakili wanalaani mashtaka ya unyanyasaji yaliyotolewa na Kinshasa, ambayo iliifungulia Rwanda mashitaka kama hayo mbele ya mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ni mtazamo “wa kipuuzi” kulingana na mratibu wa upande wa utetezi wa Rwanda.
Lakini kwa upande wa Kongo, wanasema kambi ya watuhumiwa inatumia mbinu za kuchelewesha ili kuepusha mjadala juu ya mada hiyo kwa undani. “Kupitia kesi hii, mahakama inatakiwa kuthibitisha ukuu huu wa nguvu ya sheria juu ya sheria ya nguvu na hivyo kuchangia katika uimarishaji wa mfumo wa ulinzi wa haki za binadamu barani Afrika, anahoji Profesa Ivon Mingashong… Ikizingatiwa kuwa hoja zote ambazo zimezungumzwa upande wa pili hazina msingi, ni maneno ya udhalilishaji yanayoagizwa na usanifu wa utaratibu huo. Tuna mambo ya kusema sio kulipiza kisasi, bali kuunda utaratibu wa haki, amani na udugu kwa vizazi vijavyo.”
Matokeo ya kesi hiyo yanasubiriwa, lakini bado hakuna tarehe iliyopangwa kwa mahakama kutoa uamuzi wake. Hii ni mara ya kwanza kwa mataifa mawili kukabiliana mbele ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Kibinadamu na Watu. Utaratibu huu ni sehemu ya kampeni inayoongozwa na Kinshasa katika taasisi mbalimbali za kimataifa.