
Wanaume wanne wawili raia wa Ubelgiji, mmoja wa Vietnam na Mkenya mmoja wanashikiliwa nchini Kenya kwa tuhuma za kumiliki na kufanya biashara ya kusafirisha Malkia wa Siafu walio hai.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Albane Thirouard
Hiki ni kisa cha kushangaza nchini Kenya. Watu wanne wametiwa mbaroni kwa kujaribu kuuza nje maelfu kadhaa ya Siafu walio hai kinyume cha sheria ili kuuzwa kwa wakusanyaji wa bidhaa hiyo barani Ulaya au Asia. Vijana wawili wa Ubelgiji waliokamatwa huko Nakuru katikati mwa Kenya, pamoja na Mvietnam na Mkenya mmoja huko Nairobi, wanatuhumiwa kumiliki na kusafirisha wanyamapori hai kinyume cha sheria.
Wanaume wanne ikiwemo raia wawili wa Ubelgiji, mmoja wa Vietnam na raia mmoja kutoka Kenya wanashikiliwa kwa tuhuma za kumiliki na kufanyabiashara ya kusafirisha Malkia wa Siafu walio hai 5,000 kwenye mirija 2,244 bila kibali.
Washtakiwa hao walikamatwa Aprili 5, 2025 katika maeneo tofauti, raia wa Ubelgiji walikamatwa katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Nakuru huku wengine walikamatwa Tofina Muthama Apartments, Nairobi.
Picha zilizoshirikiwa na mamlaka ya Kenya zinaonyesha mamia ya mirija ya majaribio na sindano zenye Siafu walio hai, zikiwa na pamba ili kuwaweka hai. Zaidi ya wadudu 5,000 walikamatwa, kwa thamani inayokadiriwa ya dola 7,800. Miongoni mwa Siafu hao, kuna Messor Cephalotes, aina ya mchwa wanaothaminiwa sana na wakusanyaji. Kutokana na rangi nyekundu, ukubwa wa malkia wake hadi 24 mm, na uwezo wake wa kuunda makoloni makubwa sana.
Lakini nchini Kenya, wanyama pori, wakiwemo wadudu, wanalindwa vikali… Biashara yote inahitaji vibali, ambavyo wafanyabiashara hao wanne waliokamatwa hawakuwa navyo. Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori inashutumu “uhalifu mkubwa” na operesheni “iliyopangwa”. Shirika hili la serikali linabainisha “mageuzi yanayotia wasiwasi” katika usafirishaji haramu wa “kuhama kutoka kwa mamalia nembo kwenda kwa spishi zisizojulikana, lakini muhimu kwa usawa wa ikolojia.”
Mnamo mwaka 2023, watu watatu walikamatwa nchini Kenya baada ya kujaribu kusafirisha Siafu kwenda Ufaransa kinyume cha sheria. Watu wote wanne waliokamatwa hivi majuzi wamekiri hatia. Wabelgiji hao wawili wenye umri wa miaka 19 walisema hawakufahamu kuwa kukusanya Siafu mwitu ni kinyume cha sheria.