
Nchini Kenya, wanawake hasa wenye umri mkubwa pwani ya Kenya, bado wanabaguliwa linapokuja suala la haki ya kumiliki ardhi, licha ya katiba nchini humo kuwaruhusu kufanya hivyo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa kawaida wanawake ndio hujishughulisha na utumizi wa ardhi ikiwemo ukulima, lakini wengi wao hawamiliki wala hawaridhishwi ardhi hizo. Kache Kadzo ni mkongwe wa miaka 76, alifurushwa katika ardhi ya familia yake hapa Mombasa.
‘‘Nikatoka hapa nikaenda zangu nyumbani nikija akaniambia shamba nauziwa mimi,haya pia amedhulumu, hata maskini umdhulumu kwa kuwa utajiri unazo.’’
Fatuma Musyoka ni mama aliyesaidiwa na ofisi ya serikali kupata haki yake ya ardhi.
‘‘Kuna mahali nilikuwa nimenunua ardhi nikawa nanyanyasika, mimi kidogo nimesoma najielewa nikafuatilia nikaenda kwa mzee wa mtaa, nikaenda kwa chief nikapigania huko hadi nikarudishiwa pesa yangu.’’
Halima Kulola Abdhalla, alikuwa chifu kwa miaka 22 na anawaelimisha mwanamke kuhusu ardhi .
‘‘Kuwe na uhamasisho kwa hawa akina mama maanake wengi huwa hawajui haki zao, wakinyang’anywa hivyo huwa wanakaa. Wakija wanaweza kupata usaidizi mkubwa wakaregeshwa mali zao na wakarithi.’’
Athman Fahamuni ni mshirikishi mkuu katika asasi ya kijamii ya ilishe Trust hapa Mombasa.
‘‘Wajua tena akina mama zetu wengi wao hawakusoma ama elimu yao ni chache hii imeleta sababu kuwa wamedhulima wakati wakipimiwa walikuweko lakini wakati wa kupena allotment majina yao wanafutiliwa mbali wanapewa watu wengine.’’
Inakadiriwa ni asilimia 30 ya wanawake nchini Kenya ndio wanamiliki au wamerithi ardhi. Diana Wanyonyi – MSA,rfi Kiswahili.
Diana Wanyonyi – Mombasa RFI Kiswahili