Kenya: Vyama vya Odinga na Ruto vyatiliana saini makubaliano ya ushirikiano

Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wametiliana saini, mkataba wa ushirikiano kati ya chama tawala UDA na ODM, kutatua changamoto za kijamii na kisiasa zinazowakabili wakenya.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa kinara wa upinzani na Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga na Rais William Ruto walikongamana jijini Nairobi ambapo viongozi hao walitia saini kile ambacho kimetajwa kama makubaliano ya utendakazi.

Wafuasi hao walianza kuwasili katika Ukumbi wa kimataifa wa KICC wakiwa wamevalia mavazi ya vyama vyao, wakiimba nyimbo za kuwasifia viongozi wao.

Soma piaRais Ruto na kiongozi wa upinzani Odinga wametiliana saini, mkataba wa ushirikiano

Makubaliano haya yanakuja wakati huu mapatano kati ya Odinga na Ruto yakionekana kupingwa na baadhi ya wanasiasa na raia wanaosema yanalenga kuwanufaisha wanasiasa wachahce.

Odinga amekuwa akikutana na wanachama wa chama chake cha ODM kwa ambacho alidai kwamba anapokea maoni yao kabla ya kutoa mwelekeo wake wa kisiasa.

Soma piaMaoni ya Wakenya baada ya Ruto na Odinga kutia saini mkataba wa ushirikiano

Baada ya maandamano ya vijana wa Gen Z waliokuwa wanapinga kupanda kwa ushuru wa bidhaa, Rais Ruto na Odinga walionekana kuashiria mwelekeo mpya wa muungano.

Makubaliano haya yanawakumbusha raia wa Kenya kilichofanyika mwezi machi mwaka 2018, ambapo rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta, alifanya makubaliano na Odinga.