
Kenya inaadhimisha mwaka mmoja, baada ya kuzuka kwa maandamano ya vijana maarufu kama Gen Z, kupinga mswada wa fedha wa mwaka 2024, uliopendekeza nyongeza ya kodi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katikati ya mwezi Juni mwaka 2024, maelfu ya vijana walianza kujitokeza katika miji mbalimbali hasa jiji kuu Nairobi, kushinikiza mswada huo wa fedha kuondolewa na serikali.
Maandamano hayo yaliendelea hadi Juni 25, wakati waandamanaji walipovamia majengo ya bunge, kuonesha hasira zao kwa wabunge waliokuwa wanajadili mswada huo.
Rais William Ruto, alitangaza kuachana na mswada huo Juni 26 mwaka 2025, baada ya kukubali kuwa wananchi walikuwa wameukataa.
Wakati wote wa maandamano hayo, polisi walikabiliana vikali na waandamanaji na kusababisha vifo vya watu, kwa mujibu wa Tume ya taifa ya kutetea haki za binadamu.
Watu wengine zaidi ya 80 walitekwa na maafisa na usalama, na mpaka sasa kuna baadhi ambao hawajapatikana.
Kati ya Julai 11-12, 2024, Rais Ruto alivunja baraza lake la Mawaziri na baadaye kuunda serikali mpya, iliyowashirikisha Mawaziri kutoka chama cha upinzani ODM.
Aidha Ruto, alimfuta kazi Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth Koome baada ya shinikizo za wananchi kumtaka ajiuzulu.
Septemba 20, 2024, Wanaharakati watatu waliokuwa wametekwa na kutoweka, waliachiwa huru kufuatia shinikizo za wanaharakati, na agizo la Mahakama kutaka waachiwe huru.
Mwezi Mei mwaka 2025, rais Ruto alisema mateka wote walikuwa wamerejeshwa kwa ndugu zao lakini mwanaharakati wa mitandaoni Rose Njeri alikamatwa na kufikishwa Mahakama kwa madai ya matumizi mabaya ya Kompyuta na Uhalifu wa Mtandao.
Mwanaharakati huyo, alianzisha tovuti kuwawezesha wananchi wa taifa hilo kuwaandikia barua pepe wabunge wao kuonesha kutoridhishwa kwao na baadhi ya mapendekezo kwenye mswada wa fedha wa mwaka 2025.