
Nchini Kenya, mbunge wa chama cha ODM Charles Ong’ondo Were, ameuawa hapo jana kwa kupigwa risasi jijini Nairobi, na watu waliokuwa wakilifuata gari lake.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa tarifa, mbunge huyo anayewakilisha eneo Bunge la Kasipul, alipigwa risasi na watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki kwenye barabara ya Ngong majira ya saa moja na nusu jioni.
Kifo chake kinajiri miezi miwili tangu adai kuwa masha yake yako hatarini kufuataia matukio ya ghasia katika eneo Bunge lake, ambazo alidai zilichochewa na vyanzo kutoka nje.
Kwa mujibu wa mashuhuda, mmoja wa washambuliaji hao alishuka kwenye pikipiki na kumfyatulia risasa mbunge huyo nakumjeruhi vibaya, kabla ya kukimbizwa hospitalini.
Hata hivyo, hadi kufikia sasa mazingira ya kuuawa kwa Mbunge bado zimesalia kitendawili,na tayri polisi wameanzisha uchunguzi kuwatambua wahusika.
Viongoizi mbalimbali wakiwemo spika wa bunge la taifa, Moses wentagula amekashifu kitendo hicho na kukiita cha woga.