Kenya: Mamlaka yapiga marufuku matangazo ya michezo ya kamari

Mamlaka nchini Kenya, zimepiga marufuku matangazo yote ya michezo ya Kamari kwa siku 30 kutokana na kile mamlaka zimesema matangazo hayo yamekuwa yakitumika kuwadaganya raia kwamba wanaweza pata utajiri kupitia njia ya mkato.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Bodi ya kudhibiti matangazo ya michzo ya kamari, imesema kwa siku za hivi karibuni matangazo hayo yameongezeka kwa kiasi kikubwa na kuchangia vijana wengi kujiingiza kwenye michezo ya kamari kwa imani kwamba watapata mafanikio kwa njia ya mkato.

Bodi hiyo pia imepiga marufuku matumizi ya watu mashuhuri  katika jamii kutumika kufanya matangazo ya michezo ya kamari, bodi hiyo ikielekeza kampuni zote kuwasilisha matangazo ya kamari kwa bodi ya kuthathimini ubora wa filamu nchini Kenya ili kuthiminiwa upya.

BCLB pia imeelekeza mamlaka ya mawasiliano  nchini Kenya, kuzuia matangazo ya michezo ya kamari kutoka nje ya nchi.

Hatu hii inakuja baada ya vyombo kadhaa vya habari nchini Kenya, kukadiria kwamba sekta ya michezo ya kamari nchini Kenya ilisajili faidi ya shilingi wa Kenya  billioni 766 .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *