
Mwandishi wa habari maarufu sana nchini Kenya aliyekamatwa Jumanne wiki hii na polisi baada ya kudaiwa kuchapisha habari kuhusu tuhuma za ufisadi serikalini katika wizara ya mambo ya ndani ameachiliwa huru.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Mwanahabari huyo John Ngirachu ambaye ni mhariri anayeangazia habari za bunge, anadaiwa kuandika taarifa iliyonukuu habari kutoka kwenye mkutano wa faragha wa Kamati ya Bunge kwenye gazeti la Daily Nation.
Bw Ngirachu, wa shirika la habari la Nation Media Group ameachiliwa baada ya kuandikisha taarifa na maafisa wa uchunguzi wa jinai akiwa ameandamana na mawakili wake wawili.
Baraza la wahariri limeelezea kuwa halikufurahishwa na kitendo hicho cha maafisa wa usalama nchini humo na kuomba serikali kuoboresha ushirikiano kati yake na wanahabari