
Wanafunzi wa shule ya upili ya Butere Girls iliyoko Magharibi mwa Kenya, wamekataa kuendelea na igizo lao kwa jina la ‘Echoes of War’ ambalo limezuia mjadala kwenye mitandao ya kijamii, serikali ikitajawa kuingilia.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na vyombo vya habari, wanafunzi hao walinyimwa kipaza sauti hatua ambayo iliwakasirisha na kukataa kuigiza katika mashindano ya kitaifa ambapo wameondoka ukumbuni baada ya kuimba wimbo wa taifa.
Inaripotiwa kuwa, wanafunzi hao walikataa kuonesha igizo lao hadi pale waelekezi wao ambao hawakuruhusiwa ukumbini wawepo.
Igizo la ‘Echoes of War’ imekabiliwa na pingamizi kutoka kwa serikali ya Kenya, ambapo linagusia uongozi wa Kenya na maandamano yalioongozwa na vijana wa ‘Gen Z’ mwaka wa 2024.
Awali mchezo huo ulikuwa umepigwa marufuku katika hali isioeleweka kwenye eneo la Magharibi ya Kenya kabla ya mahakama kuu kubatilisha marufuku hiyo na kuagiza wanafunzi hao kuruhusiwa kuigiza katika mashindano ya kitaifa.
Jumatano ya wiki hii, mwelekezi wa igizo hilo aliyekuwa katibu Mkuu wa chama tawala Cleophas Malala aliripoti kwamba alizuiliwa kuingia kwenye ukumbi ambapo mashindano ya mwaka huu ya shule za upili yanafanyika jijini Nakuru katika mkoa wa bonde la ufa.