Kauli ya Kagoma kwa Simba usiku

LICHA ya kutokuwa na uzoefu mkubwa kimataifa timu yake ikicheza mchezo wa kwanza hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika, kiungo Yusuph Kagoma amewatoa hofu wanasimba.

Kikosi cha Simba ambacho kilitua Misri Ijumaa ya wiki hii tayari kwa mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika mkondo wa kwanza dhidi ya Al Masry hatua ya robo fainali, kitashuka dimbani usiku wa Aprili 2, 2025.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kagoma alisema kikosi kinaendelea vizuri na mazoezi na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri huku kila mmoja akiuhitaji mchezo huo kuhusu kukosa uzoefu alisema yupo na mkongwe Ngoma ambaye amekuwa akimpa maelekezo nini afanye.

“Kikosi hakiwezi kikawa na nyota wote wazoefu ndio kifanikiwe najivunia kucheza sambamba na Ngoma ni mchezaji ambaye amefanya kila kitu kwenye mpira kwa kucheza mashindano mengi makubwa hivyo amekuwa akinijenga na kunipa maelekezo nini nifanye,” alisema na kuongeza;

“Ni mchezo mgumu ulio mbele yetu lakini sisi kwa umoja wetu kama wachezaji tumejiandaa kuhakikisha tunaipambania nembo ya klabu ili tuweze kufikia mafanikio na hilo lipo kwenye mikakati kuanzia uongozi hadi benchi la ufundi.”

Kagoma alisema anacheza kwa kujiamini akicheza sambamba na Ngoma na amekuwa akijifunza mengi kupitia mchezaji huyo hivyo haoni changamoto ya kucheza michuano hiyo migumu kwasababu yupo chini ya mchezaji bora na mzoefu.

Akizungumzia mabadiliko yakle ya uchezaji tangu ametua Simba alisema ameingia timu yenye presha kuwa anacheza kwa akili lakini pia kwa ubora ili kujihakikishia namba kikosi cha kwanza.

“Timu zote kuna ushindani wa namba lakini Simba amekutana na wachezaji wengi bora ambao wamemuongezea kasi ya kujiimarisha ili kujihakikishia nafasi chini ya kocha Fadlu Davids.”

Kagoma ametua Simba licha ya ugumu aliokutana nao kutokana na idadi kubwa ya wachezaji eneo analocheza akiwemo Debora Fernandes, Augustine Okejepha  ambao  ni usajili mpya na mkongwe Mzamiru Yassin amefanikiwa kuingia moja kwa moja kikosi cha kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *