Kauli mbiu ya Chadema “Hakuna Mageuzi, Hakuna Uchaguzi” yazua mjadala kabla ya uchaguzi wa 2025

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ametetea msimamo mkali wa chama hicho kuhusu kauli mbiu ya “Hakuna Mageuzi, Hakuna Uchaguzi” na kusisitiza kuwa umejikita katika hitaji la mfumo wa uchaguzi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katikati mwa mwezi Februari Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Upinzani Tanzania, Chadema, Tundu Lissu alisema chama hicho hakitasusia uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu na badala yake kinakwenda kuhakikisha uchaguzi huo hautafanyika kabisa.

“Chademakitaishtaki serikali ya Tanzania kwa wananchi, jumuiya za kimataifa na viongozi wa kidini ili kuhamasisha mabadiliko ya katiba na sheria za uchaguzi zinazochagiza mifumo mibaya ya uchaguzi inayovunja demokrasia”, alisema wakati huo.

Lissu aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho Januari 22 amesema mifumo ya uchaguzi Tanzania inadhibitiwa na Rais wa nchi na kwa upande wa Zanzibar pia ukidhibitiwa na Rais.

Alisema mfumo huo wa uchaguzi wa Tanzania ulisababisha Tanzania kuongozwa na viongozi ambao hawakupigiwa kura kati ya mwaka 2019/2020.