Katika mwaka 2024 mikopo kwa sekta binafsi ilikua kwa kiwango cha asilimia 12.4, hali inayodhihirisha kuimarika kwa mahusiano ka…

Katika mwaka 2024 mikopo kwa sekta binafsi ilikua kwa kiwango cha asilimia 12.4, hali inayodhihirisha kuimarika kwa mahusiano ka…

Katika mwaka 2024 mikopo kwa sekta binafsi ilikua kwa kiwango cha asilimia 12.4, hali inayodhihirisha kuimarika kwa mahusiano kati ya sekta ya fedha na sekta za uzalishaji, kwa mujibu wa Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo.

Ameongeza kuwa sekta ya kilimo imeongoza kwa kupokea sehemu kubwa ya mikopo hiyo, ikiwa na asilimia 41 ya jumla ya mikopo yote kwa sekta binafsi.

Matokeo haya, kwa mujibu wa Waziri, ni kiashiria cha mwelekeo chanya wa ukuaji wa uchumi, na yanaonesha jinsi Serikali ilivyojipanga kuimarisha mazingira rafiki kwa wawekezaji wa ndani na wa nje, hasa kupitia sera thabiti za fedha na mipango ya maendeleo.

✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *