Katika kuadhimisha Siku ya Baba Duniani, wanaume mkoani Singida wamehimizwa kuwa na uwajibikaji katika familia kwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika malezi na mahitaji ya familia zao.
Viongozi wa jamii na wadau wa maendeleo wameonya tabia ya baadhi ya wanaume kuzitelekeza familia na kuwaachia wanawake mzigo wa kulea watoto peke yao, hali inayodhoofisha ustawi wa familia na jamii kwa jumla.
#azamnewsupdates
✍Deus Liganga
Mhariri| @official_jennifersumi