Katibu Mkuu wa UN: Hakuna kisingizio cha kuikosesha Afrika kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, hakuna kisingizio cha kuifanya Afrika iendelee kuwa haina uwakilishi wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.