Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameagiza kuheshimiwa kwa ardhi na uhuru wa DRC akionya pia dhidi ya mzozo wa Congo kugeuka kuwa wa kikanda.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Matamshi yake katika kikao cha wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika unaofanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia ameyatoa wakati huu waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wakiingia katika Mji wa Bukavu Kivu Kusini.
Mzozo wa DRC umepewa kipau mbele katika kikao hicho, shinikizo la kimataifa likiendelea dhidi ya Rwanda kusaidia katika usitishaji wa mapigano mashariki ya DRC.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ameonekana akihudhuria mkutano huo wakati mwenzake wa DRC Tshisekedi akikosa kutokana na hatua ya waasi wa M23 kuingia katika Mji wa Bukavu.

Hatua ya waasi wa M23 kuingia katika Mji wa Bukavu imejiri baada ya kuingia katika Mji mwengine wa Goma kivu Kaskazini. Wakiwa mjini Goma walidaiwa kudhibiti uwanja wa ndege wa Goma kabla ya kuelekea katika Mji jirani wa Bukavu.
Umoja wa Afrika umetuhumiwa kwa namna ambavyo umeshugulikia mzozo wa mashariki ya DRC, ukitakiwa kuchukua hatua dhabiti kudhibiti hali.
Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wale Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe nane ya mwezi huu kwa kauli moja walitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano nchini DRC, makabiliano yakirejelewa tena siku ya Jumanne ya wiki hii.