Katibu Mkuu wa UN aahidi Afrika kuwa na mwakilishi wa kudumu kwenye Baraza la Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema sio sawa kwa bara la Afrika kutokuwa na kiti cha mwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na ameahidi kufanya kazi na Umoja wa Afrika na nchi wanachama ili kuhakikisha kuwa nchi za Afrika zinapata mwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama.