Katibu Mkuu wa Hizbullah: Tutaendeleza njia ya Sayyid Hassan Nasrullah hata kama sote tutauawa

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema katika mazishi na shughuli ya kuisindikiza miili ya Mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiyyuddin, Makatibu Wakuu wa harakati hiyo ya Muqawama waliouawa shahidi kwamba: “tutashikamana na ahadi tuliyotoa na tutaendeleza njia ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah hata kama sote tutauawa”.