
KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Juma Kaseja ameshtushwa na mfululizo wa matokeo mabaya ya kikosi chake kilichopoteza mechi mbili mfululizo za ligi huku akikiri mambo yanazidi kuwa magumu kwao.
Katika hesabu za kujinasua na janga la kushuka daraja, kocha huyo amesema ana mechi mbili ngumu sawa na dakika 180 dhidi ya Azam na Simba ambazo anaona zimeshikilia hatma yao.
Kagera Sugar imetoka kupoteza dhidi ya Tanzania Prisons kwa bao 1-0 kisha ikachapwa 2-0 na Dodoma Jiji, mechi zote zimepigwa