Karibu wagonjwa 1,200 zaidi wa kipindupindu wameripotiwa katika jimbo la White Nile, Sudan

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa kesi 1,197 za ugonjwa wa kipindupindu, vikiwemo vifo 83 vilivyosababishwa na ugonjwa huo vimesajiliwa katika jimbo la White Nile siku mbili zilizopita.