Karibia marais 40 wa Afrika wamewasili nchini Ethiopia kwa mkutano wa AU

Marais wa Afrika wanawasiili jijini Addis leo kwa kikao maalum  cha umoja huo ambapo tamko la pamoja kuhusu hali mashariki mwa DRC litatolewa  na baadaye kushiriki kura za uenyekiti wa tume ya Umoja  wa Afrika.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Baada ya mawaziri wa mataifa 49 kufanya uchaguzi wa makamishna sita wa tume wa AU,marais kesho wanatazamiwa kushiriki kikao  ambacho kitakuwa cha  faragha ambacho kitatangulizwa na kujadiliwa kwa ripoti  kuhusu  hali ya usalama baada ya kikao cha EAC na SADC.

Rais wa Kenya William Ruto anatazamiwa kushiriki kikao cha jioni na viongozi hao wa Afrika, wakiwa pamoja na Raila Odinga ambapo watatoa tamko kuhusu wakimbizi wa mapigano wa mashariki mwa DRC

Musalia Mudavadi ni waziri wa mashauriano ya kigeni nchini Kenya.

 Tuna uthibitisho wa marais 35 ambao wataongoza nchi zao,wengine watakuwa ni mawaziri wakuu,manaibu rais au mawaziri wa mambo ya nje”amesema Musalia Mudavadi.

Katika kura ambayo itafanyika kwa njia ya siri, kati ya wagombea watatu Mahamoud Ali wa Djibouti, Raila Odinga kutoka Kenya na Richard Randriamandrato atachaguliwa kumrithi Moussa Faki Mahamat raia wa Chad.

Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika anayeondoka.
Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika anayeondoka. © AFP

Lakini uchaguzi huu una maana gani kwa raia wa nchi mbali mbali?

Dkt Ibrahim Assane Mayaki amekuwa ni kamishena maalum wa AU, Anatokea Niger ukanda wa Sahel ambao umeshuhudia pia usalama mdogo na migogoro ya kisiasa

 Katika kila mfumo wa Umoja wa Afrika swala la mzozo sharti kushughulikiwa,pili kuna swala nataka nilitaje ambalo ni la wafugaji,wawe wanatokea Afrika Mashariki au Afrika Magharibi,wameathirika na mabadiliko ya tabia nchi na wanalazimika kuhama hama na mifugo na kukwazana na wanajamii wengine  na hili pia lilezua mzozo mkubwa.”AmesemaDkt Ibrahim Assane.

Umoja wa Afrika una mataifa wanachama 55 ila Umoja huo ulisitisha uanachama wa nchi sita ikiwemo Burkina Faso,Guinea ,Gabon ,Niger   Mali, na Sudan kutokana na mapinduzi yaliyofanyika nchi hizo.

Carol Korir, Addis Ababa RFI KISWAHILI