Kapo ya Aziz KI, Hamisa Mobeto yawania tuzo

SIKU chache baada ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI kufunga ndoa na mwanamitindo, Hamisa Mobetto kapo yao imewekwa kuwania tuzo.

Wanandoa hao wanawania tuzo ya Africa Golden Awards katika kipengele cha kapo bora ya mwaka tuzo zitakazotolewa, Aprili 5 mwaka huu huko Kenya.

Aziz KI na Hamisa wamechaguliwa kuwania tuzo hiyo ambayo pia wanashindania mastaa kibao kutoka Afrika.

Mastaa hao watachuana na mastaa wengine wa Tanzania, akiwemo muigizaji Zaylissa & Haji Manara, Vanessa Mdee na Rotimi (Nigeria), Priscilla Ojo& Juma Jux.

Mastaa wengine ni Davido & Chioma (Nigeria) ambao walifunga ndoa mwaka jana, Amberay & Kennedy Rapudo (Kenya), Kateclinton & Vincent Mackay (Rwanda), The WA Jesus Family (Kenya) na The Mamideb and Cleave (Uganda).

Zari Hassan & Shakib Cham (Afrika Kusini, Uganda), The Mziza’s (Kenya), Ruby & Mocmadu (Nigeria), Miss Michuki & Jordan Lee (Kenya), Vanessa & Brad (Kenya, Marekani), Diana Marua na Bahati wa Kenya na Mr & Mrs Phoenix (Zimbabwe).