Kampuni ya China kuwekeza katika ujenzi wa reli kati ya Tanzania na Zambia

Kampuni ya uhandisi ya Uchina, sasa itawekeza kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.4 kwa ajili ya kuboresha njia ya reli kati ya Tanzania na Zambia, uwekezaji utakaosaidia kurahisisha usafiri wa watu na mizigo.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Njia hiyo ya reli inayofahamika kama Tazara, inatarajiwa kuwa njia kuu ya usafirishaji madini hasa ya shaba na Kobalt katika mataifa ya kusini mwa Afrika.

Mwaka jana China ilitia saini kandarasi ya kuifufua upya reli hiyo yenye karibu miaka 50, ikijaribu kushindana na Marekani ambayo akielekea tamati ya uongozi wake, ras Joe Biden alitoa kiasi cha dola milioni 550 kujenga reli toka Angola hadi DRC kwenye bandari ya Lobito.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, dola bilioni moja zitatumika kufanya maboresho ya reli ya Tazara, huku kiwango kilichosalia kikitarajiwa kutumika kununua vichwa vya treni 32 na mabehewa 762 ili kuijengea uwezo.

Mkataba huu kati ya Tazara na Uchina utadumu kwa miaka mitatu na utagawanya katika awamu ya miaka mitatu ya ujenzi na miaka 27 ya uendeshaji na matengenezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *