Kamanda wa Marekani akiri kusalia matupu maghala ya silaha ya nchi hiyo

Kamanda wa jeshi la Marekani katika eneo la Indo- Pacific amekiri kuwa maghaala ya silaha ya nchi hiyo hivi sasa yapo matupu.

Samuel Paparo amesema kuwa vita na mapigano huko Ukrane na katika eneo la Asia Magharibi yamepelekea kusalia matupu maghala ya silaha ya Marekani.

Paparo ameongeza kuwa: “Matumizi ya kijeshi ya Marekani yameitwisha nchi hiyo gharama kubwa kwa ajili ya kujiandaa kukabiliana na mizozo barani Asia na Pasifiki, hasa ikizingatiwa kuwa China ni adui mwenye nguvu zaidi wa Marekani duniani.

Serikali ya Biden kwa muda sasa inatuma silana na mifumo ya ulinzi wa anga ya kisasa huko Ukraine na Israel. Hivi karibuni jeshi la Marekani lilituma mfumo wa ulinzi dhidi ya makombora wa THAAD katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).