KAMANDA WA MAKOMNADOO WA URUSI:TUMEWALIZA UKRAINE

 Naibu mkuu wa Kurugenzi Kuu ya Kijeshi-Siasa ya Kikosi cha Wanajeshi wa Urusi na kamanda wa kitengo maalum cha Akhmat Apty Alaudinov

 

“Tuliondoa shehena moja ya kivita na silaha moja ya kujiendesha yenyewe, kisha tukalipua kituo cha kuhifadhia silaha ambapo magari kadhaa ya kijeshi yalihifadhiwa,” aliandika kwenye Telegram. “Tuliilipua muda mfupi baada ya upelezi wetu kugundua.”.

“Wakati wa wiki hii, vitengo vya kundi la vita vya Kaskazini viliendelea na operesheni ya kufuta uvamizi wa Kiukreni katika Mkoa wa Kursk. Katika mashambulizi ya ana kwa ana na kwa kutumia ndege,makombora na ndege zisizokuwa na Rubani tulifanikiwa kuwaangamiza wanajeshi wa Ukraine waliojitokeza na kujiandaa kukabiliana nasi na tukafanikiwa kukomboa  jumuiya za Uspenovka na Borki .zilikombolewa na zipo chini ya himaya yetu.”

“Katika wiki hiyo iliyopita, adui walipoteza hadi askari 3,510, vifaru 18, ikiwa ni pamoja na kikiwemo kifaru cha Leopard 2  kutoka  Ujerumani, magari ya kivita 117, magari 66, mifumo miwili ya kurusha makombora, ikiwa ni pamoja na moja ya Marekani, na mifumo ya mizinga 34. pia kituo cha vita vya kielektroniki kiliharibiwa,” ilisema.

 

Kando na hayo, kulingana na kamanda huyo, ndege za Urusi zilishambulia maeneo ya kupeleka wanajeshi  na silaha za jeshi la Ukraine lililokuwa na silaha kali za kivita, kifaru kimoja, brigedi mbili za mashambulio, na vile vile vikosi viwili vya ulinzi wa eneo kuzuia majaribio ya kukabiliana na uimarishaji wa mashambulizi toka upande wetu. “Pia  magari ya jeshi la Ukraine  na vikosi vya baharini, pamoja na vikosi vitatu vya ulinzi wa eneo vilipigwa katika maeneo ya Volchansk na Liptsy,” Alimalizia kamanda huyo.