Kamanda Mkuu wa US Ulaya: Mauzo ya silaha za Marekani kwa Ulaya yameongezeka kwa 600%

Kamanda Mkuu wa Marekani katika Kamandi ya jeshi la nchi hiyo barani Ulaya amesema, mauzo ya silaha za Marekani kwa nchi za Ulaya yameongezeka kwa asilimia 600 tangu vilipoanza vita kati ya Russia na Ukraine na akaongeza kuwa, thamani ya kiwango cha silaha zilizoagizwa na nchi za Ulaya tangu vilipoanza vita kati ya Russia na Ukraine hadi sasa imefikia dola bilioni 265.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *