
KOCHA Mkuu wa KMC, Kali Ongala amepata ushindi wake wa tatu ndani ya timu hiyo katika kipindi cha siku 139 tangu akabidhiwe kikosi hicho Novemba 14, 2024 akichukua nafasi ya Abdihamid Moallin aliyetimkia Yanga.
Katika mechi hizo zote tatu alizoshinda, zimechezwa uwanja wao wa nyumbani wa KMC uliopo Mwenge, Dar es Salaam.
Ushindi wa kwanza kwa kocha huyo ulikuwa Desemba 16, 2024 wa bao 1-0 dhidi ya Pamba Jiji kupitia bao la Hance Masoud dakika ya 88.
Baada ya hapo, akakaa kwa siku 56 Februari 10, 2025 aliposhinda tena mabao 2-0 dhidi ya Singida Black Stars mfungaji akiwa Oscar Paul dakika ya 35 na 40, kisha Aprili 2 akaichapa Tanzania Prisons 3-2 kwa mabao ya Shaban Idd Chilunda dakika ya 41 na 66, huku Ibrahim Elias akifunga dakika ya 55.
Akizungumza na Mwanaspoti, Ongala alisema licha ya kuibuka na ushindi dhidi ya Tanzania Prisons, timu yake haikucheza vizuri kutokana na kushindwa kulinda vizuri nyavu zao zisitikiswe.
“Nimefurahi timu yangu imepata matokeo mazuri lakini bado nina kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha haya yanayotokea sasa hayajirudii kwenye mechi zilizo mbele yetu, nitakaa na wachezaji wangu kupanga mipango sahihi ya kumaliza mechi sita zilizobaki,” alisema na kuongeza.
“Timu ili iweze kupata matokeo mazuri inatakiwa kujengwa kuanzia eneo la ulinzi kwani washambuliaji wanaweza wakatumia nafasi walizotengeneza lakini wakaangushwa na safu ya ulinzi, ndicho kilichotokea, lakini huu sio wakati wa kulaumiana nitahakikisha timu inabadilika kila eneo na kuwa na ushindani hasa kwenye mechi zilizobaki ambazo zina umuhimu kwetu ili kujitengenezea mazingira mazuri mwisho wa msimu.”
Kocha huyo tangu akabidhiwe kikosi cha KMC