
KAGERA Sugar imemaliza ukame wa ushindi baada ya kushinda nyumbani wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate ikiwa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba huku mshambuliaji raia wa Uganda, Peter Lwasa akifunga penalti mbili zilizoiwezesha wenyeji kupata ushindi wa tatu msimu huu.
Kabla ya mchezo huo uliopigwa jioni ya leo, Kagera ilikuwa imecheza mechi nane bila kushinda kwangi mara ya mwisho kupata ushindi ilikuwa Novemba 4, 2024 ilipoichapa Dodoma Jiji kwa mabao 2-1 kwenye uwanja huo huo wa Kaitaba.
Hata hivyo matokeo hayo hayajaisaidia Kagera kutoka nafasi ya 15, licha ya kufikisha pointi 15 baada ya mechi 19 ilizocheza hadi sasa.
Katika mchezo huo, Kagera ilianza kuonyesha dhamira ya kupindua meza mapema kwa kupata bao la kwanza kwa penalti dakika ya 23 iliyofungwa na Peter Lwasa kabla ya dakika ya 34 kuongeza bao jingine la mkwaju kama huo na kumfanya afikishe mabao saba hadi sasa katika ligi hiyo. Penalti hizo zilitolewa na mwamuzi Japhet Smart baada ya mabeki wa Fountain kufanya madhambi langoni mwao na kufanya mabao hayo yadumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili mambo yalionekana kama yangeisha kwa wenyeji kuondoka na ushindi wa mabao hatyo mawili, lakini dakika za lala salama beki Saleh Seif Kambenga alidunga bao la tatu na kuizima kabisa Fountain Gaste inayonolewa na Mkenya Robert Matano ikiwa haijaonja ushindi wowote chjini yake hadio sasa zaidi tya sare ya 1-1 na Simba.
Hilo lilikuwa ni bao la pili kwa beki huyo, lakini Fountain inaweza kuwa na kisingizio kwa kipigo hicho kutokan na kuumia kwa kipa namba moja wao, John Noble dakika ya 16 na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Parapanda. Noble alikuwa amerejea kikosi baada ya kukosa mechi iliyopita waliolala mabao 2-0 baada ya awali kulimwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Simba.
Hata hivyo Parapanda naye baada ya kuruhusu mabao mawili akashindwa kumalizia mchezo akiumia dakika ya 87 na nafasi yake ikabidi ichukuliwe na kiungo Mtenje Albano ambaye alianza mchezo kwa kupangua mashuti mawili makali kabla ya kuruhusu bao la mwisho la wenyeji.
Fountain Gate imeendelea kupepesuka ikishindwa kupata ushindi katika mechi ya sita mfululizo kwenye ligi tangu iliposhinda 3-2 Desemba 13,2024 dhidi ya Coastal Union, lakini ikirudia tukio la kumtumia mchezaji wa ndani kukaa langoni baada ya makipa wao kupata matatizo.
Katika mchezo dhidi ya Simba beki Hashim Omary akilazimika kukaa langoni baada ya Noble John kutolewa kwa kadi nyekunddu iliyotokana na kuonyesha kadi ya pili ya njano, baada ya kumaliza idadi ya wachezaji wa kuwabadilisha kama ilivyotokea tena leo mbele ya Kagare kwa beki Mtenje Juma kukaa langoni.