Kagera Sugar hali si shwari

KAGERA Sugar ina kibarua cha kupambana ili kuepuka kushuka daraja kutokana na mambo yalivyo kwa upande wao msimu huu katika Ligi Kuu Bara.

Kagera juzi usiku ikiwa nyumbani ilipokea kipigo cha mbao 2-1 kutoka kwa Tabora United na kuiacha isalie katika nafasi ya 15, ikiwa na jumla ya pointi 12 tu kupitia mechi 18, baada ya kushinda michezo miwili na kutoka sare nane na kupoteza michezo 10, ikuifunga mabao 13 na kufungwa 27.

Matokeo hayo yanazidi kuiweka pabaya Kagera ikitofautiana pointi tatu na wanaoburuza mkia, KenGold ya Mbeya ili na pointi tisa katika mechi 18.

Kwa sasa Kagera imesaliwa na mechi 12 za kuamua hatma yao ya kuendelea kuwepo Ligi Kuu kwa msimu ujao au kuwafuata ‘ndugu’ zao Mtibwa Sugar ambao walishuka msimu uliopita baada ya kudumu katika ligi hiyo tangu ilipopanda daraja mwaka 1996.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Kagera ilipanda daraja mwaka 2005, ikiwa na maana ina miaka 20 bila kushuka daraja na sasa ina kibarua cha kupata matokeo mazuri ili kuendelea kukamua katika ligi hiyo ya juu kwa ngazi za klabu nchini. Kumbuka timu hiyo imewahi kutumikiwa na wachezaji mastaa mbalimbali akiwamo, Mrisho Ngassa, Obrey Chirwa, Ben Karama, Paul Kabange, Maregesi Magwa, OPaul Kabange, Juma Jabu, Omar Changa, Katrume Songoro, Mike Katende, Vicent Barnabasr, Yusuf Macho na wengineo, mbali na kunolewa na makocha kama  Abdallah Kibadeni, Jackson Mayanja, Sylvester March na wengineo.

Kwa sasa Kagera ipo chini ya kocha Mmarekani Melis Medo baada ya kumtema  Paul Nkata aliyempokea Fred Felix ‘Minziro’ aliyekuwa nayo msimu uliopita, huku ikiwa imeongeza sura kadhaa mpya katika dirisha dogo, lakini mambo yakiwa bado magumu kwao.

Kagera hii msimu wa 2016-2017 ilikaribia kidogo kushangaza mashabiki kwa kumaliza nafasi ya tatu katika msimamo, nafasi bora zaidi kwa mabingwa hao wa zamani wa Kombe la Tukser 2006, ilipoifunga Smba kwa mabao 2-1 katika fainali Agosti 20, 2006 kwenye wa Taifa (sasa Uhuru).

New Content Item (1)
New Content Item (1)

MECHI 12 ZA KIBABE

Kagera imesaliwa na mechi 12 za kibabe ambazo kama itashindwa kuzitumia vyema itakula kwao ukiwamo ujao dhidi ya Fountain Gate kabla ya kuvaana na KenGold na JKT Tanzania.

Pia kuna KMC, Pamba Jiji, Coastal Union, Tanzania Prisons, Dodoma Jiji, Azam, Mashujaa,

Namungo na ile ya mwisho dhidi ya Simba.

Katika mechi hizo, Kagera itacheza tano kati ya hizo nyumbani na zilizosalia zitakuwa za ugenini ikiwamo hiyo ya Simba.

18 ZILIZOPITA

Kageka katika mechi 18 ilizocheza zikiwamo mbili za hivi karibuni dhidi ya Singida BS iliyotoka nao sare ya 2-2 na ya juzi iliyofumuliwa nyumbani 2-1 na Tabora, rekodi zinaonyesha katika mechi nyingine 16 zilizopita ilipoteza nje ndani kwa Yanga kwa kufungwa 2-0 na 4-0.

Ililala kwa Simba kwa mabao 5-2 nyumbani, ikatoka sare ya 1-1 na Namungo, huku na TZ Prisons,

Mashujaa 1-1 Kagera, ikalala 1-0 kwa Azam, ikaichapa Dodoma Jiji (2-1), Coastal Union (1-1), Pamba (1-1), ikalazwa 1-0 na KMC, kisha kupigwa 3-1 na Fountain Gate.

Ikaishinda KenGold kwa mabao 2-0, ikatoka suluhu na JKT Tanzania, ikalazwa mapema na Tabora United kwa bao 1-0 sawa na na ile ya Singida BS. Katika mechi hizo 18 imeshinda mbili tu dhidi ya Dodoma Jiji na KenGold zote ikicheza nyumbani mwaka jana, ikiwa na maana kwa mwaka huu haijaonja ushindi wowote katika ligi hiyo.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

MSIMU WA  2023/24

Mashujaa 2-0 Kagera Sugar (Agosti 16), Ihefu 1-0 Kagera Sugar (Agosti 19), Kagera Sugar  1-0 Geita Gold (Septemba 17), JKT Tanzania 1-1 Kagera Sugar Sugar (Septemba 29), Kagera Sugar 1-1 Namungo (Oktoba 4) na Mtibwa Sugar 0-2 Kagera Sugar (Oktoba 19).

Nyingine Dodoma Jiji 1-0 Kagera Sugar(Oktoba 25), Kagera Sugar  0-0 Tabora United (Oktoba 30),Kagera Sugar  2-1 Tanzania Prisons(Novemba 3),Kagera Sugar 1-1 KMC (Novemba 22),

Kagera Sugar 0-0 Yanga(Feb 2),Simba 3-0 Kagera Sugar(Desemba 15),Coastal Union 1-0 Kagera Sugar(Desemba 9), Kagera Sugar 0-4 Azam (Desemba 21).

Kagera Sugar 1-0 Singida BS(Feb 12),Kagera Sugar1-1 Mashujaa(Feb 16),Kagera Sugar 2-1 Ihefu(Feb 25),Geita Gold  0-0 Kagera Sugar(Feb 28),Kagera Sugar 1-1 JKT Tanzania(Machi 2),Namungo1-0 Kagera Sugar(Machi 5),Kagera Sugar 0-0 Mtibwa Sugar(Machi 10),Kagera Sugar1-1 Dodoma Jiji (Aprili 13),Tabora United 0-3 Kagera Sugar(Aprili 17),Tanzania Prisons 0-0 Kagera Sugar (Aprili 22),KMC 0-0 Kagera Sugar(Mei 4),Yanga1-0 Kagera Sugar(Mei 8)

Kagera Sugar 1-1 Simba(Mei 12),Kagera Sugar 1-2 Coastal Union(Mei 21), Azam 5-1 Kagera Sugar(Mei 25), Singida BS 2-3 Kagera Sugar(Mei 28).

Ilimaliza nafasi ya 10 katika mechi 30 ilishinda saba, sare 13, ilifungwa mechi 10, ilikusanya pointi 34, mabao ya kufungwa 32 ya kufunga 23.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

WASIKIE WADAU

Kocha wa zamani wa timu hiyo, aliyewahi pia kuinoa Simba, Jackson Mayanja maarufu kama Mia Mia, anasema timu hiyo kuwa nafasi ya pili kutoka mkiani haimaanishindio imeshuka daraja, anaamini bado ina kitu cha kufanya ili iendelee kusalia.

Alishauri uongozi wa timu hiyo kama kuna mambo hayapo sawa wayatengeneze na kuhakikisha wanakuwa kitu kimoja kuipigania isishuke kutokana na heshima ya ukongwe wake katika ligi, tangu ilipopanda 2005.

“Kati ya timu ambazo naendelea kuzikumbuka katika ligi ya Tanzania miongoni ni hiyo  Kagera, katika mechi ilizobakiza kufunga msimu huu ziwekewe mikakati imara, kwa maana ya wachezaji, makocha na viongozi kila mmoja awajibike ipasavyo katika majukumu yake,” anasema Mayanja aliyewahi pia kuinoa Coastal Union.

“Ligi ya Tanzania ni ngumu inayohitaji mipango madhubuti kwa kila klabu hasa mzunguko wa pili ambao unakuwa wa kutimiza malengo, ndio maana nasema viongozi wakae wajue wanafanya kitu gani kunijisuru na kushuka daraja.”

Anasema waanze kusaka pointi kwa mechi 12 zilizosalia ili kujiweka pazuri.

“Jambo la kwanza iwe sare kisha watafute pointi tatu wasiruhusu kufungwa hilo linaweza likasaidia zaidi kusalia katika ligi,” anasema Mayanja na kuongeza;

“Kipindi nafundisha Kagera Sugar niliamini katika vijana, ushirikiano ulikuwa mkubwa kutoka kwa viongozi hasa kunisajilia wachezaji ninaowahitaji, naipenda sana hiyo timu na viongozi wakinitaka nitarudi Tanzania,”anasema Mayanja na kuongeza;

“Japo sijaifuatilia Ligi ya Tanzania ila sitarajii Kagera ishuke daraja, kikubwa viongozi waangalie ni kitu gani kinaleta changamoto katika timu wakitatue kwa umoja.”

Nahodha wa zamani wa timu hiyo, George Kavila anachokiona ni upepo ambao kuna wakati timu inakuwa na umoja wa uwajibikaji wa majukumu kama viongozi, wachezaji na makocha.

“Namba moja wanaotakiwa kuhakikisha timu inasalia Ligi Kuu ni wachezaji wenyewe, vingozi na makocha baada ya hapo watajua kipi kinawaangusha wakifanyie kazi, Kagera ni timu kongwe iliyokuwa na ushindani mkali nina uzoefu tangu nilipoichezea 2007-2019,” anasema.

Anasema tangu Kagera ilipopanda Ligi Kuu 2005 hadi 2025 siyo jambo dogo, hivyo ni suala la viongozi na wachezaji kulizingatia hilo.

“Kipindi nafundisha Kagera Sugar niliamini katika vijana, ushirikiano ulikuwa mkubwa kutoka kwa viongozi hasa kunisajilia wachezaji ninaowahitaji, naipenda sana hiyo timu na viongozi wakinitaka nitarudi Tanzania,”anasema Mayanja na kuongeza;

“Japokuwa sijaifuatilia Ligi ya Tanzania ila sitarajii Kagera ishuke daraja, kikubwa viongozi waangalie ni kitu gani kinaleta changamoto katika timu wakitatue kwa umoja.”

New Content Item (1)
New Content Item (1)

WACHEZAJI HAWA HAPA

Kipa wa timu hiyo Ramadhan Chalamanda, baada ya kufungwa dhidi ya Yanga alitoa kauli ya mashabiki wawaombee kutokana na wakati mgumu wa kupata matokeo ya ushindi.

Kwa upande wa beki mkongwe wa timu hiyo, David Luhende anasema; “Tupo nafasi mbaya lakini tutapambana hadi tone la mwisho kuhakikisha inabaki, ingawa siyo kazi rahisi ila inatubidi.”

NAFASI KATIKA LIGI

2024-2025- 15

2023-2023- 10

2022-2021- 11

2020-2021- 12

2019-2020- 8

2018-2019- 18

2017-2018- 9