Jumuiya ya mateka wa Palestina: Mateka 58 wamekufa shahidi katika muda wa miezi sita iliyopita

Mkuu wa Jumuiya ya mateka wa Palestina amesema, kuna hatari nyingi zinatishia maisha ya mateka wa Kipalestina, na kwamba katika kipindi cha miezi sita iliyopita, mateka 58 wamekufa shahidi wakiwa ndani ya jela za utawala wa Kizayuni.