Jumuiya ya ASEAN na udharura wa kusaidia kutatua mgogoro wa Waislamu wa Rohingya

Sambamba na mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mashhauri ya Kigeni wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) huko Langkawi, Malaysia, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo amesisitiza dhamira ya Kuala Lumpur kama mwenyekiti wa zamu wa umoja huo juu ya kutatuliwa mgogoro wa Myanmar na kurejesha amani ya nchi hiyo.