Julio aapa kitaeleweka Berkane

Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ni miongoni wa Wanasimba ambao wameambatana na timu hiyo kuja hapa Morocco kwa ajili ya mechi ya kwanza ya hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu huu dhidi ya RS Berkane, Jumamosi ijayo.

Mechi hiyo itachezwa saa 1:00 usiku kwa saa za hapa ikiwa ni sawa na saa 4:00 usiku kwa muda wa Tanzania na Kihwelo ametamba kuwa anaona Simba ikiandika historia katika hatua hiyo.

Julio amesema kuwa maandalizi ambayo yanaendelea kufanywa na Simba yanampa matumaini kuwa itafanya vizuri katika mechi dhidi ya Berkane.

“Mechi ya fainali sio rahisi kwetu Simba kwa sababu tunacheza na timu ngumu na itakuwa katika uwanja wa nyumbani lakini kwa haya maandalizi ninayoyaona, nina imani mambo yatakuwa mazuri.

“Mechi hii ya kwanza huku ugenini ndio muhimu zaidi kupata matokeo mazuri ili kazi tukaimalizie nyumbani,” alisema Julio.

Julio ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba na kocha wa timu hiyo alisema kuwa wachezaji wanapaswa kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa mashindano hayo msimu huu ili kufuta historia mbaya ya timu hiyo kukosa Kombe la CAF mwaka 1993.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *