Juhudi za Trump za kufutililia mbali mpango wa kuundwa nchi huru ya Palestina

Kuongezeka misaada ya silaha ya Rais Donald Trump wa Marekani kwa Israel pamoja na mpango wake wa kuwahamisha kwa nguvu wakazi wa Ukanda wa Gaza na kuwapeleka Misri na Jordan kunaonyesha kuwa moja ya vipaumbele vyake ni kubadili ramani ya eneo hilo na kuharibu kabisa mpango wa kuanzisha nchi huru ya Palestina.