
Rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila, ambaye tangu mwaka jana makazi yake yalikuwa ni nchini Afrika Kusini, hapo jana kwa mara nyingine alivunja ukimya na kutangaza kuwa hivi karibuni atarejea nchini mwake.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Katika taarifa yake, rais Kabila ametaja kuzorota kwa hali ya usalama na nia yake ya dhati ya kutaka kusaidia mchakato wa kuleta amani ya gudumu mashariki mwa nchi hiyo, kama mambo yaliyochangia afanye uamuzi wa kurudi nyumbani.
Katika barua iliyoonwa na idhaa ya RFI, rais Kabila amesema baada ya kuwa nje ya nchi yake kwa miaka 6, anaamini muda umefika wa yeye kurejea nyumbani haraka kwa kuzingatika yanayoendelea.
Licha ya kuwa katika barua yake hakusema ni lini hasa atarejea, watu wake wa karibu kisiasa wameidokeza idhaa hii kuwa huenda ikawa ni hivi karibuni.
Rais Kabia kwenye taarifa yake ameongeza kuwa atakaporejea ataanzia katika êneo la mashariki mwa nchi hiyo, bila hata hivyo kuweka wazi ni jimbo gani atakaloanzia, huku akithibitisha kuwa na mazungumzo na viongozi wa maeneo hayo.
Kwa wadadisi wa mambo tangazo lake la kurejea nyumbani linaibua maswali kadhaa, moja ni kwanini sasa hivi? Ni vipi aamue kuanzia katika êneo la mashariki mwa Kongo? Je huenda ana mawasiliano na aliyewahi kuwa mwenyekiti Wake wa tume ya uchaguzi Corneille Nangaa, ambaye sasa ni kiongozi wa AFC/M23 akiongoza êneo la Goma na Bulkavu
Barua yake imetolewa wakati huu chama chake cha PPRD kikitangaza kurejea kwa nguvu katika siasa za nchi hiyo kwa kukataa kushirikia majadiliano ya kitaifa yaliyoitishwa na rais Felix Tshisekedi.