
Dar es Salaam. Hakuna mwaka Miss Tz iliotesha mastaa kama 2006. Baada ya hapo haikuwa Miss Tz tena. Bali zilikuwa tafrija za Miss Tz. ‘Pati’ za kusaka mwakilishi wa nchi Miss World.
Washiriki wakataka Uwema Sepetu zaidi na siyo Umiss Tz.
Halikuwa na mashiko tena, mambo yakaharibika zaidi. Na watoto wa kike wakaanza kuona sehemu sahihi ni kwenye filamu.
Ni baada ya kuona hata mamiss wanahamia kwenye filamu. Kila pisi ikataka uigizaji, muziki, utangazaji na ‘uvideo kwini’. Hakuna aliyetaka kuwa Flaviana wala Magesse. Wote wakawa wehu wa kuigiza.
Kabla ya Umiss wa 2006. Ilikuwa fahari kuu mtoto kushiriki Umiss. Baadaye ikawa fedheha kwa familia mtoto kushiriki Umiss. Waandaaji wakaanza kukosa warembo wenye viwango.
Wenye viwango walianza kuhofia kudhalilisha familia. Shindano likakosa mvuto na warembo wenye mvuto. Likakosa mvuto kwa watu na kukosa mvuto kwa wadhaamini. Habari ikaishia hapo.
Lundenga kupitia Miss Tanzania, alizalisha mastaa wengi wa kike. Ruge kupitia radio naye alizalisha mastaa wengi wa kike. Kanumba pia kupitia filamu alizalisha mastaa wengi sana wa kike.
Ruge na Kanumba wametangulia mbele ya haki. Lakini mazao yao bado yanafifaidisha jamii. Anko Hashim yupo hai lakini shindano lake limepoteza uhai. ‘Viasi Vesa’.