Jeshi la Yemen langusha ndege ya kivita ya Marekani aina ya MQ-9 Reaper

Vikosi vya ulinzi wa anga vya Yemen vimelenga kwa kombora na kuiangusha ndege nyingine ya kivita ya Marekani  isiyo na rubani aina ya MQ-9 Reaper katika mkoa wa kaskazini wa al-Jawf, ikiwa ni ndege ya 12 ya aina hiyo kuangusha na vikosi vya nchi hiyo.

Vyombo vya habari vya Yemen vimeripoti kwamba ndege hiyo isiyo na rubani ilidunguliwa ilipokuwa ikifanya operesheni ya ujasusi katika  eneo hilo mapema Ijumaa

Video zilizosambaa mtandaoni zilionekana kuonyesha ndege ikidondoka kutoka angani ikiwa inateketea moto katika eneo la mkoa wa al-Jawf nchini Yemen.

Jeshi limethibitisha kuangusha ndege hiyo ya kisasa ya Marekani inayogharimu dola milioni 30.

Mnamo Septemba 30, Msemaji wa Jeshi la Yemen (YAF) Brigedia Jenerali Yahya Saree alisema vikosi vya Yemen viliidungua ndege isiyo na rubani ya MQ-9 Reaper ya Marekani katika mkoa wa kaskazini-magharibi wa Sa’ada.

Saree alisema katika taarifa ya televisheni wakati huo kwamba ndege hiyo isiyo na rubani lililengwa kwa kombora lililotengenezwa kienyeji kutoka ardhini hadi angani.

Wananchi wa Yemen wametangaza uungaji mkono wao wa wazi kwa mapambano ya Palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel tangu utawala huo ghasibu ulipoanzisha vita vya kutisha dhidi ya Gaza tarehe 7 Oktoba mwaka jana na kuua Wapalestina wasiopungua 43,469 hadi sasa.

Jeshi la Yemen, katika kutii matakwa ya wananchi,  limesema kuwa halitasimamisha mashambulizi yake dhidi ya Marekani na Israel na waitifaki wao had mashambulizi ya anga na ya anga ya Israel huko Gaza yatakapomalizika.

Kiongozi wa harakati ya muqawama ya Ansarullah ya Yemen Abdul-Malik al-Houthi amesema ni “heshima na baraka kubwa kukabiliana na Marekani moja kwa moja.”