Jeshi la Wanamaji la Iran linafuatilia kwa karibu meli za kivita za Marekani

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu yaIran amepongeza ufuatiliaji wa kina wa kikosi hicho juu ya meli za kivita za Marekani zinazosafiri katika maji ya eneo.

Akizungumza Jumatatu  Admeri Shahram Irani alisema meli kubwa ya kivita ya Marekani yenye kusheheni ndege pamoja na meli manoari zingine  16 za Marekani zilizopo katika maji ya eneo zinafuatiliwa mara kwa mara  ndege zisizo na rubani za upelelezi wa kijeshi za Iran.

Tuko juu ya vichwa vyao,” aliongeza, akiashiria meli za kivita za Marekani

Amesema ndege hizo za upelekezi za jeshi la Iran zinaonekana wazi na hazijajificha na hiyo ni njia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwaambia Wamarekani  kwamba eneo hili sio mahali penu.”

Admeri Shahram Irani amesema ni nukta muhimu sana kwamba Iran ina uwezo wa kumchunguza na kumfuatilia adui hata baharini,” huku akibainisha kuwa jambo hili limegeuka kuwa “sababu ya wasiwasi kwa Wamarekani.”

Admeri Shahram Irani

Kamanda huyo alilipongeza Jeshi la Wanamaji kwa kufanikiwa kulinda meli zote za Iran na zile za nchi ambazo zimeaomba msaada wa kusindikizwa meli zao

Akifafanua nukta hiyo amesema: Jeshi la Wanamaji la Iran linasindikiza shehena za mafuta na biashara kutoka ufuo wa Venezuela hadi Amerika, Ulaya, na Afrika, na kukabiliana na ukiukaji wowote unaoweza kufanyika dhidi ya meli za Iran.”