Jeshi la Uganda laelekea katika moja ya miji yakaskazini mashariki mwa DRC

Jeshi la Uganda limethibitisha siku ya JumapiliMAchi 2, 2025 kwamba limetuma wanajeshi katika mji mwingine wa kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupambana na makundi yenye silaha atika eneo hilo, huku kukiwa na hofu kwamba mzozo mkali unaweza kuongezeka na kuwa vita vikubwa zaidi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Wanajeshi wetu wameingia katika mji wa Mahagi na tunaudhibiti,” msemaji wa masuala ya ulinzi na kijeshi wa Uganda Felix Kulayigye ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili.

Jeshi la Kongo liliombwa na jeshi la Kongo kufuatia mauaji ya raia yanayodaiwa kufanywa na wanamgambo wanaojulikana kwa jina la Cooperative for the Development of Congo (Codeco), amesema bila kutoa maelezo zaidi.

Mahagi iko  katika mkoa wa Ituri, ambao unapakana na Uganda, ambapo takriban watu 51 waliuawa mnamo Februari 10 na watu wenye silaha wanaohusishwa na kundi la Codeco, kulingana na vyanzo vya kibinadamu na vya ndani.

Codeco inadai kutetea masilahi ya jamii ya Lendu, inayoundwa zaidi na wakulima, dhidi ya jamii ya Hema, inayoundwa zaidi na wafugaji.

Uganda tayari ina maelfu ya wanajeshi katika maeneo mengine ya Ituri chini ya makubaliano na serikali ya Kongo.

Mwezi uliopita, Uganda ilitangaza kwamba wanajeshi wake “wamechukua udhibiti” wa mji mkuu wa mkoa wa, Bunia.

Ituri iko kaskazini mwa mkoa wa Kivu Kaskazini na Kusini, ambayo iliangukia chini ya udhibiti wa kundi linaloipinga serikali la M23, linaloungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda, mwishoni mwa mwezi wa Januari.

Wachambuzi wanahofia kuwa kuongezeka kwa uwepo wa wanajeshi wa Uganda na Rwanda mashariki mwa DRC kunaweza kusababisha kurudiwa kwa Vita vya Pili vya Kongo vilivyodumu kuanzia mwaka 1998 hadi 2003, na kuhusisha nchi nyingi za Afrika na kusababisha mamilioni ya vifo kutokana na ghasia, magonjwa na njaa.